Sunday 24 August 2014

"WAFUNGWA WAISHTAKI SERIKALI YA BOTSWANA KUDAI HAKI YA KUPATIWA ARV"


Mahakama kuu ya Nchini Botswana imeamuru serikali ya nchi hiyo kuwapatia dawa za kupunguza makali ya Virusi vya ukimwi,raia wote wa kigeni wanaotumikia vifungo kwa makosa mbalimbali nchini humo na gharama zote ziwe ni juu ya serikali ya  nchi hiyo.

    Hali hiyo imefuatia baada ya raia wawili wa Zimbabwe,Dickson Tapela na Mbuso Piye wanaotumikia kifungo nchini Botswana kuishtaki serikali hiyo kwa kukataa kuwapatia huduma ya dawa za kupunguza makali ya ukimwi.

No comments:

Post a Comment