Tuesday 26 August 2014

"MABINTI WA UMRI WA MIAKA 5 WANAOZWA ILI KUJIKWAMUA NA UGUMU WA MAISHA"

Mmoja wa wanaume katika ndoa na binti aliye chini ya miaka 19,huu ni mfano tu wa ndoa hizo nchini Ethiopia.






















Nchini Ethiopia wazazi wanaoshindwa kuzihudumia familia zao huwaoza mabinti zao katika umri mdogo sana,hali hiyo huwapelekea vifo vya mimba za utotoni.Mwanamke mmoja anaejulikana kama Merkedes Murgeta ambaye hakumbuki hata tarehe ya ndoa yake,lakini ndugu zake wanamkumbusha kwamba aliolewa akiwa na miaka mitano (5).


Mugeta anaeishi katika kijiji cha Mosebo kilichopo mkoani Amhara katikati ya nchi ya Ethiopia.Katika eneo hili kama ilivyo kawaida kwenye maeneo mengine ya Ethiopia,ni kosa kuolewa chini ya miaka 18.Kutokana na takwimu za USAID,Amhara inatajwa kama sehemu ambapo ndoa za utotoni zimekithiri kuliko maeneo yote duniani.


"VIPAUMBELE VYA WANASIASA" 
"Nchi imeweka kipaumbele kikuu kwenye afya ya mama mjamzito na mtoto" 

No comments:

Post a Comment