Thursday 31 July 2014

Watu 6,740 kuwania nafasi 47 za kazi TBS

Usaili huo unataka kufanana na ule wa Idara ya Uhamiaji ambao ulihusisha waombaji 10,000 waliokuwa wakiwania nafasi 70, utafanyika leo na kesho katika Ukumbi wa Yombo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
FUATILIA HAPA

Friday 25 July 2014

NATENGENEZA ZAIDI YA MILION 50,UFUGAJI WA KUKU NA NGURUWE


Nikiwa natembea kando ya barabara kando kando ya barabara ya Saza mjini Iganga,nilisikia kundi la waendesha boda boda wakimuongelea Prof.Mmoja anaefuga Kuku na Nguruwe.Nikajikuta nimevutiwa na mazungumzo yao.Niliguswa na namna walivyokuwa wakitazama kazi ile kama ya Aibu na Mbaya  kabisa kwa mtu wa nafasi ile kujihusisha na ufugaji.

KWA HABARI ZAIDI INGIA HAPA

Tuesday 22 July 2014

''MAPAPAI YAMENIPATIA KILA NINACHOMILIKI''


Jina langu ni  Nelson Ssemwogerere,mkazi wa kijiji cha Walubira,Wilaya ya Mukono.Mimi ni mfanya biashara wa Papai na Nanasi.Nimekuwa nikilima haya mazao mawili kwa muda wa miaka 10.Lakini kabla sijaingia kwenye kazi hii nilikua nalima Kahawa kama zao kuu la kuniingizia kipato.Lakini baada ya miche yangu ya Kahawa kuharibiwa na magonjwa,nikawa najiuliza ni zao lipi litalopandwa kuchukua nafasi ya Kahawa.Kuharibiwa kwa bustani yangu kulileta masumbuko kwa sababu ilikua ndio chanzo changu kikuu cha pesa.
KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Saturday 19 July 2014

NAFASI ZA KAZI,JARIBU BAHATI YAKO HAPA

Wenye fani za ICT,Afya,Mazingira,Biashara Wanaopenda kufanya kazi katika mashirika mbalimbali ya kimataifa waweza jaribu bahati yako hapa.
INGIA HAPA

KUTANA NA KIJANA ALIYEAMUA KUJIHUSISHA NA KILIMO CHA MATIKITI





Pamoja na kazi ya ufugaji aliyoifanya kwa muda mrefu,anasema alichoshwa na kusubiri chakula cha msaada kutoka Serikalini hasa msimu ambao mvua zinasumbua.
  ''Kuna siku tumeshinda bila kula kwa sababu tulikosa chakula.Ilibidi tuhame hapa na pale ili kutafuta  chakula chetu na pia kulisha  mifugo yetu,lakini tangu tukaribishe kilimo,tumetatua tatizo''.Kwa mwezi Muhammed anapata Kshs 20,000 kwa kuuza Matikiti na Ndizi.Lakini anaongeza kwa kusema ''Unyonyaji kutoka kwa madalali,wadudu waharibifu na upungufu wa wataalamu wa kilimo ni kati ya changamoto wanazokumbana nazo..
     INGIA HAPA KWA HABARI ZAIDI

Friday 18 July 2014

TUZUNGUMZE:MAFANIKIO NI NINI?


Nini maana halisi ya neno mafanikio au kufanikiwa?,Je ni kuwa na nyumba nyingi?,kusaidia wasiojiweza?,ni kuwa mbinafsi?,ni kuwa mchoyo?,je ni kusaidia makundi ya wasiojiweza?..
Mafanikio ni kupata kile ambacho ulipanga kukipata.WEWE ndiye unaeweza kupanga mafanikio yako yaweje kutokana na jinsi unavyotaka.Mafanikio hayategemei na mtazamo wa mtu mwingine zaidi ya mtazamo wako.Mafanikio hayawezi kupimwa kutokana na idadi ya vitu ulivyonavyo (Materialistic Measurement).

       
     Ingawa  nyakati nyingine mafanikio ya mtu yanaweza kupimwa kwa idadi ya  vitu mtu alivyonavyo,kama pesa au nyumba mpya. Mafanikio yanaweza kuwa ni Ubinafsi, kama Madaraka na Ukatili unaotokana na kuwa na cheo fulani.

Mafanikio yanaweza kuzungumziwa kwa mtazamo wa hisia Mf kupata umpendae/kufunga pingu za maisha.

Mafanikio pia yanaweza kuwa hali ya kutokua mbinafsi na kuwa na moyo wa upendo kwa jamii yote inayokuzunguka,kama vile kuona watoto wote wakiwa na Afya bora,na Salama,wakipata Mlo ulio bora nk.Hakuna njia moja ya kuelezea mafanikio,zaidi ya maelezo yaliyotangulia hapo juu.Mafanikio yana maana tofauti kwa kila mtu.
  Hata hivyo waliofanikiwa wote wanafanana kwa jambo moja nalo ni DHAMIRA ya dhati.Ili ufanikiwe,huna budi kwanza kuweka Dhamira iliyo thabiti.

                           KUAMINI
     Ili mafanikio yapatikane yanapitia michakato miwili ambayo ni  DHAMIRA na  IMANI,ambavyo vyote kwa pamoja vinaanza katika fikra zetu.Kwa mtindo huu tutakuwa tunajitengenezea fursa na machaguo (Opportumities and Choices).Badili namna unavyofikiri kuanzia sasa,na utabadili mazingira yako na utabadili maisha ya uwapendao,na jamii nzima kwa ujumla.Niwatakie ijumaa njema waungwana,ningependa niwaache na ujumbe huu wa kujenga zaidi.

''MACHO YATAKUWA HAYANA MAANA KAMA FIKRA ZETU ZITAKUWA NA UPOFU'' '' THE EYES ARE USELESS IF OUR MIND IS BLIND''.
INGIA HAPA KWA HABARI ZAIDI

Wednesday 16 July 2014

Luis Suarez: BARCELONA WASEMA WAMESHAMSAINISHA MSHAMBULIAJI WA LIVERPOOL

Luis Suarez ni mchezaji wa Barcelona kwa 100%,Barcelona wamethibitisha hilo.Kwa uhamisho wa paund milion 75 kwa makubaliano yaliyofanyika wiki iliyopita.Hata hivyo Barcelona hawataweza kumuonesha mchezaji huyo mbele ya mashabiki wa timu hiyo kama ilivyo desturi yao,kutokana na Suarez 27  kutumikia adhabu ya miezi minne kutojihusisha na shughuli zozote zinazohusiana na kandanda kwa kosa la kumng'ata  beki wa Italy Giorgio Chiellini,wakati wa Fainali za kombe la dunia 2014.   Luis Suarez

INGIA HAPA KWA HABARI ZAIDI

Monday 14 July 2014

MARADONA AFUNGUKA ''MESSI HAKUSTAHILI TUZO''

Maradona kama mojawapo ya mtu anayeheshimika kwenye soka katika nchi yake ya Argentina na ulimwengu mzima,amesema Messi hakustahili tuzo ya Mpira wa dhahabu inayojulikana kama ''Golden Ball Award''.Messi,27 alitajwa kama mchezaji bora wa mashindano ingawa walifungwa na Ujerumani 1-0 katika fainali zilizofanyika Jumapili uwanja wa Maracana.

Argentina forward Lionel Messi (right) and Germany keeper Manuel Neuer

LIVERPOOL :BADO KIDOGO KUNASA SAINI YA LAZAR MARKOVIC

Lazar Markovic mwenye umri wa miaka 20,anaefanyiwa vipimo ndani ya klabu ya liverpool wanapokaribia kumsaini winga Mserbia anaechezea klabu ya Benfica.Ada  ya uhamisho inakadiriwa kufikia  paundi milioni 20.
    Wakati huo huo klabu ya liverpool inasubiri uamuzi wa straika wa Lille Divock Origi,mwenye umri wa miaka 19.

            Lazar Markovic

Sunday 13 July 2014

UJERUMANI WAVISHWA UBINGWA WA DUNIA KWA MARA YA NNE HUKU MARIO GOTZE AKIPELEKA KILIO ARGENTINA

Mario Gotze akitokea benchi kwa mara ya kwanza anaweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga goli la ushindi katika fainali za kombe la dunia akitokea benchi katika muda wa ziada dakika ya 113,na kuibuka shujaa kwa kuamua matokeo ya mechi ya leo.Mafanikio haya yanamaanisha Ujerumani imekuwa timu ya kwanza kutoka bara la Ulaya  kushinda kombe katika ardhi ya Amerika ya kusini


Wakati huo huo James Rodriguez amabaye ni mshambuliaji wa Colombia  ashinda kiatu cha dhahabu kwa kuibuka mfungaji bora wa  kwa kombe la dunia 2014,kwa kuifungia timu yake mabao sita 6
.


       KWA HABARI ZAIDI SOMA HAPA.http://www.bbc.com/sport/0/football/28181689

Saturday 12 July 2014

HUYU NDIYE REFARII ATAKAECHEZESHA FAINALI YA KOMBE LA DUNIA MWAKA 2014

Nicola RizzoliNicola Rizzoli

REFA MUITALIANO NICOLA RIZZOLI NDIYE REFARII ALIYECHAGULIWA NA FIFA KUICHEZESHA FAINALI YA KOMBE LA DUNIA YA MWAKA 2014 KATI YA GERMANY NA ARGENTINA ITAKAYOFANYIKA SIKU YA JUMAPILI YA TAREHE 13 MWEZI JULAI.

REFARII HUYO MWEYE UMRI WA MIAKA 42 PIA ALIWEZA KUCHEZESHA MECHI KATI YA HISPANIA NA UHOLANZI, NIGERIA NA ARGENTINA NA PIA ALICHEZESHA MECHI KATI YA ARGENTINA NA UBELGIJI KATIKA FAINALI HIZI ZA KOMBE LA DUNIA 2014.

FAINALI HIYO ITACHEZWA JUMAPILI SAA 4 USIKU KATIKA KIWANJA CHA MARACANA JIJINI RIO DE JANEIRO NCHINI BRAZIL.




Friday 11 July 2014

MRITHI WA SUAREZ LIVERPOOL APATIKANA


 WILFRIED BONY

LIVERPOOL INAMTAKA STRAIKA WA SWANSEA CITY NA IVORY COAST WILFRIED BONY KUWA MRITHI WA LUIS SUAREZ AMBAYE ANAELEKEA BARCELONA.

NYOTA HUYO WA IVORY COAST ALIYEIFUNGIA CLUB YAKE YA SASA, SWANSEA CITY MABAO 25 MSIMU ULIOPITA ANA THAMANI YA EURO MILIONI 19 TU. NYOTA HUYO WA IVORY COAST AMEWAAMBIA RAFIKI ZAKE KUWA ATAFURAHI SANA KAMA LIVERPOOL WATAKUBALI KUTOA HIYO ADA ILI KUMNASA.

HABARI ZINASEMA BONY, HANA FURAHA KATIKA KLABU HIYO YA SWANSEA CITY NA YUPO TAYARI KUHAMA.

ANGEL DI MARIA ANUKIA MANCHESTER UNITED

Angel di Maria Argentina
                 NYOTA WA ARGENTINA NA REAL MADRID : ANGEL DI MARIA

RIPOTI ZINASEMA NYOTA WA ARGENTINA NA REAL MADRID ANGEL DI MARIA AMEKUBALI KUTUA MANCHESTER UNITED NA KWAMBA ATAKUA ANALIPWA MSHAHARA WA EURO 150,000 KWA WIKI MOJA.

MAN UTD WANATAKA KUTOA ADA YA EURO MILIONI 30 AMBAYO NI EURO MILIONI 10 PUNGUFU KWANI REAL MADRID WANATAKA UERO MILIONI 40.

NYTOTA HUYO MWENYE UMRI WA MIAKA 26 KWA SASA YUPO BRAZILI NA TIMU YAKE YA TAIFA YA ARGENTINA AMBAYO INASUBIRI KUCHEZA FAINALI JUMAPILI.

INGIA HAPA KWA HABARI ZAIDI

ARSENAL YAMNASA NYOTA WA CHILE

Alexis Sanchez Arsenal
ALEXIS SANCHEZ


TIMU YA ARSENAL IMEKAMILISHA USAJILI WA MSHAMBULIAJI WA CHILE NA BARCELONA ALEXIS SANCHEZ KWA DAU LA EURO MILIONI 35 JANA JIONI.

NYOTA HUYO WA CHILE ALIYEWIKA SANA KWENYE FAINALI YA KOMBE ZA DUNIA AMEKUA MCHEZAJI GHALI WA PILI NYUMA YA MESUT OEZIL ALIYESAJILIWA NA KLABU HIYO YA LONDON

                                                  . INGIA HAPA KWA HABARI ZAIDI

Thursday 10 July 2014

WACHEZAJI WENYE THAMANI YA £67M WAMEKARIBIA ARSENAL


Alexis Sanchez Chile

ALEXIS SANCHEZ

HIZI ZINAWEZA KUWA HABARI NZURI KWA MASHABIKI WA TIMU YA ARSENAL AMBAYO INASEMEKANA KUKARIBIA KUFANYA USAJILI WENYE THAMANI YA EURO MILIONI 67. HABARI ZINARIPOTI KUWA USAJILI HUO UNAWEZA KUKAMILIKA NDANI YA SAA 48 ZIJAZO. WACHEZAJI AMBAO WANAKARIBIA KUTUA ARSENAL NI ALEXIS SANCHEZ MWENYE THAMANI YA EURO MILIONI 32, LOIC REMY MWENYE THAMANI YA EURO MILIONI 8, MATHIEW DEBUTCHY WA NEWCASTLE UNITED MWENYE THAMANI YA EURO MILIONI 11 NA WA MWISHO NI LARS BENDER WA BAYER LEVERKUSEN MWENYE THAMANI YA EURO MILIONI 22. 

SWALI NI JE? HAWA NDO WACHEZAJI AMBAO ARSENAL WANAWAHITAJI KUSHINDA TAJI LA LIGI KUU YA UINGEREZA?













SAMIR NASRI AONGEZA MKATABA MPYA MAN CITY

Samir Nasri Manchester City

SAMIR NASRI



KIUNGO WA ZAMANI WA ARSENAL, SAMIR NASRI AMEONGEZA MKATABA MPYA NA KLABU YAKE YA SASA (MAN CITY),

KIUNGO HUYO MWENYE UMRI WA MIAKA 27 AMESAINI MKATABA MPYA NA KLABU YAKE HIYO YA MAN CITY LEO MCHANA, MKATABA AMBAO UTAFANYA AWE HAPO MAN CITY HADI JUNE 2019.

SAMIR NASRI ALIMALIZA MSIMU ULIYOPITA KWA KUSHINDA TAJI LA LIGI KUU NA ALIKUA MMOJA KATI YA WACHEZAJI WALIYOISAIDIA TIMU HIYO KUTWAA UBINGWA KWA KUIFUNGIA MABAO MANANE NA KUTOA PASI 11 ZA MWISHO.

INGIA HAPA KWA HABARI ZAIDI

MIKE TYSON ASEMA ANAELEWA KWANINI LUIS SUAREZ ALIMNG'ATA GIORGIO CHIELLINI

Mike Tyson

     MIKE TYSON 

MIKE TYSON ASEMA, UNG'ATAJI WA SUAREZ KWA CHIELLINI HAIKUA KITU KIKUBWA KWANI ILIKUA NI WAKATI TU WA STRESS NA KUPANIKI KWA MCHEZAJI NA HUWA INATOKEA MARA KWA MARA KATIKA MICHEZO YA AINA ZOTE ULIMWENGUNI. 
"FIFA WAMEFUNGIA SUAREZ KUCHEZA SOKA KWA MIEZI MINNE LAKINI HIYO HAIKUA ADHABU NZURI KWANI NI KITU CHA KAWAIDA TU KUTOKEA ENDAPO MCHEZAJI ATAKUA AMEPANIKI AU YUPO KWENYE STRESS" ALISEMA BONDIA HYO WA ZAMANI.

LAKINI PIA HATA YEYE NI MTU WA MATUKIO KAMA HILO LA LUIS SUAREZ AMBAPO MWAKA 1997 ALIMNG'ATA BONDIA MWENZAKE EVANDER HOLYFIELD.

"WAKATI MWINGINE KATIKA MASHINDANO UNAWEZA KUWA MTU AMBAYE SIYO WEWE NA UKAFANYA VITU TOFAUTI NA UKAWAIDA. SO NAELEWA NI KWANINI LUIS SUAREZ ALIMNG'ATA GIORGIO CHIELLINI": alisema bondia hyo wa zamani mwenye umri wa miaka 48.



JE UNAUJUA WIMBO MPYA WA CHRIS BROWN ALOWASHIRIKISHA RICK ROSS PAMOJA NA USHER RAYMOND?




SIKU CHACHE BAADA YA CHRIS BROWN KUTOKA JELA AMEACHIA WIMBO MPYA AKIWASHILIKISHA RICK ROSS PAMOJA NA USHER RAYMOND. NYOTA HUYO WA MUZIKI WA R&B ANAONEKANA KURUDI KWA KASI KWANI NI WASANII WACHACHE SANA AMBAO HUWA WANAWEZA KUTOKA JELA NA KUACHIA NYIMBO NZURI KAMA WALIVYOKUA WAKIACHIA HAPO AWALI. TUMEONA WASANII KADHAA AMBAO WAO PIA WAMEONEKANA KUISHIWA MAKALI YAO BAADA YA KUTOKA JELA.

JE UNAUJUA WIMBO HUU MPYA WA MUIMBAJI HUYU WA LOYAL? KAMA HUUJUI BASI NI WAKATI WAKO KUJUA NI NINI AMEIMBA KATIKA WIMBO HUO WA NEW FLAME!

SIKILIZA NA KUDOWNLOAD WIMBO HUO HAPA:

CLICK HERE





HABARI NZURI KWA MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED

Enzo Perez SL Benfica

TIMU YA MANCHESTER UNITED IMETOA OFFER YA EURO MILIONI 7 ILI KUMNASA KIUNGO MACHACHARI WA ARGENTINA ANAYE CHEZEA TIMU YA BENFICA YA URENO. RIPOTI KUTOKA VYOMBO VYA HABARI VYA URENO VIMESEMA KWAMBA MAN UTD WAMEWEKA MEZANI OFFER HIYO YA EURO MILIONI 7 ILI KUMNASA KIUNGO HUYO MWENYE UMRI WA MIAKA 28 NA SASA WANASUBIRI JIBU KUTOKA BENFICA KAMA WANAWEZA KUNASA SAINI YA PEREZ.


http://www.caughtoffside.com/2014/07/10/manchester-united-make-7m-bid-for-benficas-world-cup-midfield-star/#more-315814

SWALI KWA MASHABIKI WA MAN UTD, JE HUU NDIO USAJILI UNAOFAA SASA?