Friday 5 September 2014

"KATIKA KARNE YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA,MAJI NI ANASA NA SIO HITAJI LA MUHIMU LA BINADAMU"

Baada ya miaka 30 ya njaa iliyokithiri nchini Ethiopia,bado upatikanaji wa maji ni wa mashaka hasa ukizingatia umuhimu weneyewe wa maji kwa binadamu kama usemi maarufu usemao maarufu ''MAJI NI UHAI''.Ikiwa asilimia 52 ya watu wote inapata huduma bora za maji lakini,asilimia 10 pekee ndio waliounganishiwa bomba hadi majumbani mwao.Katika maeneo ya vijijini ni asilimia 1 tu  iliyounganishwa na huduma hii muhimu katika maisha ya binadamu..


KWA HABARI ZAIDI>>>

Hii ina maana kubwa sana.Kwa nchi ambayo uchumi wake unategemea Kilimo,upungufu wa maji hauathiri Uchumi pekee bali  unaathiri maisha ya kila siku ya wakazi hawa ambao kujikimu kwao kunategemea mavuno ya kila msimu.Mara nyingi nchi maskini kama ya Ethiopia,yenye wakazi wengi,inakumbwa sana na janga la kukosekana kwa huduma ya maji.


Kuna mambo mengi yanayochangia ukosefu wa maji safi na salama,kuanzia uharibifu wa Mazingira unaosababishwa na ukataji ovyo wa miti,majanga ya kiasili kama Mafuriko na mabadiliko ya tabia nchi....!!!


No comments:

Post a Comment