Sunday 13 July 2014

UJERUMANI WAVISHWA UBINGWA WA DUNIA KWA MARA YA NNE HUKU MARIO GOTZE AKIPELEKA KILIO ARGENTINA

Mario Gotze akitokea benchi kwa mara ya kwanza anaweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga goli la ushindi katika fainali za kombe la dunia akitokea benchi katika muda wa ziada dakika ya 113,na kuibuka shujaa kwa kuamua matokeo ya mechi ya leo.Mafanikio haya yanamaanisha Ujerumani imekuwa timu ya kwanza kutoka bara la Ulaya  kushinda kombe katika ardhi ya Amerika ya kusini


Wakati huo huo James Rodriguez amabaye ni mshambuliaji wa Colombia  ashinda kiatu cha dhahabu kwa kuibuka mfungaji bora wa  kwa kombe la dunia 2014,kwa kuifungia timu yake mabao sita 6
.


       KWA HABARI ZAIDI SOMA HAPA.http://www.bbc.com/sport/0/football/28181689

No comments:

Post a Comment