Friday 18 July 2014

TUZUNGUMZE:MAFANIKIO NI NINI?


Nini maana halisi ya neno mafanikio au kufanikiwa?,Je ni kuwa na nyumba nyingi?,kusaidia wasiojiweza?,ni kuwa mbinafsi?,ni kuwa mchoyo?,je ni kusaidia makundi ya wasiojiweza?..
Mafanikio ni kupata kile ambacho ulipanga kukipata.WEWE ndiye unaeweza kupanga mafanikio yako yaweje kutokana na jinsi unavyotaka.Mafanikio hayategemei na mtazamo wa mtu mwingine zaidi ya mtazamo wako.Mafanikio hayawezi kupimwa kutokana na idadi ya vitu ulivyonavyo (Materialistic Measurement).

       
     Ingawa  nyakati nyingine mafanikio ya mtu yanaweza kupimwa kwa idadi ya  vitu mtu alivyonavyo,kama pesa au nyumba mpya. Mafanikio yanaweza kuwa ni Ubinafsi, kama Madaraka na Ukatili unaotokana na kuwa na cheo fulani.

Mafanikio yanaweza kuzungumziwa kwa mtazamo wa hisia Mf kupata umpendae/kufunga pingu za maisha.

Mafanikio pia yanaweza kuwa hali ya kutokua mbinafsi na kuwa na moyo wa upendo kwa jamii yote inayokuzunguka,kama vile kuona watoto wote wakiwa na Afya bora,na Salama,wakipata Mlo ulio bora nk.Hakuna njia moja ya kuelezea mafanikio,zaidi ya maelezo yaliyotangulia hapo juu.Mafanikio yana maana tofauti kwa kila mtu.
  Hata hivyo waliofanikiwa wote wanafanana kwa jambo moja nalo ni DHAMIRA ya dhati.Ili ufanikiwe,huna budi kwanza kuweka Dhamira iliyo thabiti.

                           KUAMINI
     Ili mafanikio yapatikane yanapitia michakato miwili ambayo ni  DHAMIRA na  IMANI,ambavyo vyote kwa pamoja vinaanza katika fikra zetu.Kwa mtindo huu tutakuwa tunajitengenezea fursa na machaguo (Opportumities and Choices).Badili namna unavyofikiri kuanzia sasa,na utabadili mazingira yako na utabadili maisha ya uwapendao,na jamii nzima kwa ujumla.Niwatakie ijumaa njema waungwana,ningependa niwaache na ujumbe huu wa kujenga zaidi.

''MACHO YATAKUWA HAYANA MAANA KAMA FIKRA ZETU ZITAKUWA NA UPOFU'' '' THE EYES ARE USELESS IF OUR MIND IS BLIND''.
INGIA HAPA KWA HABARI ZAIDI

No comments:

Post a Comment