Tuesday, 26 August 2014

"MABINTI WA UMRI WA MIAKA 5 WANAOZWA ILI KUJIKWAMUA NA UGUMU WA MAISHA"

Mmoja wa wanaume katika ndoa na binti aliye chini ya miaka 19,huu ni mfano tu wa ndoa hizo nchini Ethiopia.






















Nchini Ethiopia wazazi wanaoshindwa kuzihudumia familia zao huwaoza mabinti zao katika umri mdogo sana,hali hiyo huwapelekea vifo vya mimba za utotoni.Mwanamke mmoja anaejulikana kama Merkedes Murgeta ambaye hakumbuki hata tarehe ya ndoa yake,lakini ndugu zake wanamkumbusha kwamba aliolewa akiwa na miaka mitano (5).


Mugeta anaeishi katika kijiji cha Mosebo kilichopo mkoani Amhara katikati ya nchi ya Ethiopia.Katika eneo hili kama ilivyo kawaida kwenye maeneo mengine ya Ethiopia,ni kosa kuolewa chini ya miaka 18.Kutokana na takwimu za USAID,Amhara inatajwa kama sehemu ambapo ndoa za utotoni zimekithiri kuliko maeneo yote duniani.


"VIPAUMBELE VYA WANASIASA" 
"Nchi imeweka kipaumbele kikuu kwenye afya ya mama mjamzito na mtoto" 

Monday, 25 August 2014

"BIASHARA YA NYAMA YA PANYA INAWAINUA WENGI NCHINI CAMBODIA"

Panya wanaotegwa kutoka mashamba ya mpunga,inafikiriwa kuwa ni bidhaa adimu nchini Cambodia.

Mavuno ya kipekee yanayoendelea kwenye mashamba ya mpunga nchini Cambodia ambapo makumi elfu ya panya pori wanategwa wakiwa hai  kila siku,huku wakisafirishwa kwenda nje ya nchi hiyo.


LADHA YAKE NI SAWA NA KITIMOTO

Baadhi ya watumiaji wa nyama hiyo ya panya wanasema inafanana na ladha ya nyama ya Nguruwe,maarufu kama Kitimoto kama inavyotambulika katika baadhi ya maeneo mengi ya nchini Tanzania.








Sunday, 24 August 2014

"WAFUNGWA WAISHTAKI SERIKALI YA BOTSWANA KUDAI HAKI YA KUPATIWA ARV"


Mahakama kuu ya Nchini Botswana imeamuru serikali ya nchi hiyo kuwapatia dawa za kupunguza makali ya Virusi vya ukimwi,raia wote wa kigeni wanaotumikia vifungo kwa makosa mbalimbali nchini humo na gharama zote ziwe ni juu ya serikali ya  nchi hiyo.

    Hali hiyo imefuatia baada ya raia wawili wa Zimbabwe,Dickson Tapela na Mbuso Piye wanaotumikia kifungo nchini Botswana kuishtaki serikali hiyo kwa kukataa kuwapatia huduma ya dawa za kupunguza makali ya ukimwi.

Saturday, 23 August 2014

"WANANCHI WANA HASIRA KWA PESA ZINAZOTUMIKA KUJENGA UWANJA WA SOKA BADALA YA KUJENGA MAKAZI"

Wananchi wana hasira na serikali yao,kwa kutumia  mabilioni ya  pesa kujenga uwanja wa soka,badala ya kujenga makazi ya wananchi

Baadhi ya wakazi 4800 wasio na makazi wametengeneza kambi karibu na uwanja wenye thamani ya Dola milioni 350,katika jiji la Sao Paulo wakidai  kujengewa nyumba.


















"UONGO KUHUSU KUPUNGUZA UMASKINI WAANIKWA"

Kampeni ya maendeleo ya Milenia imetangaza kwamba umaskini duniani umepunguzwa kwa nusu ya matarajio kuelekea 2015.

Busara zinazokuja  kutoka kila upande:Viwango vya umaskini vinapungua na umaskini uliopindukia utakomeshwa muda si mrefu.Benki ya Dunia,Serikali ya nchi Matajiri na zaid ya yote kampeni  za milenia za Umoja wa mataifa wote wanakubaliana na wazo hili.Muwe watulivu,ndivyo wanavyotuambia.


Ni hadithi ya kuliwaza,lakini kwa bahati mbaya haina ukweli.Umaskini hautokomei kwa kasi kama inavyozungumzwa.Kinyume chake,kutokana na baadhi ya vipimo,umaskini umekuwa ukiongezeka kwa kasi kubwa sana inayotisha.




Thursday, 21 August 2014

"MADAKTARI 300 WA HOSPITALI YA TAIFA YA KENYATA 'KNH' WAGOMA KUFANYA KAZI ,KISA MSHAHARA WA JULAI"

Madaktari ndani ya Hospitali ya Taifa ya Kenyata,KNH,wakianza mgomo 21/08/2014,Nje ya Ofisi ya Wizara ya Afya Wakidai Mshahara wa mwezi Julai.

Janga linainyemelea nchi ya Kenya,baada ya madaktari 314 waliosajiliwa katika hospitali ya Taifa ya Kenyatta kuingia mtaani kudai mshahara wa mwezi Julai.

Aidha madaktari hao walioamua kuandamana siku hii ya leo ya Alhamisi (21/08/2014),kutoka KNH kwenda jengo la Afya kisha kuelekea Bungeni.


Wakati huo,Bungeni Dr James Nyikal,ambaye alikuwa mkurugenzi wa huduma za kitabibu ambaye ndiye Mbunge wa Seme aliitisha kikao cha dharula kuangalia namna ya kutatua kilio hicho...























"Di MARIA AMEWAAMBIA REAL MADRID ANATAKA KUONDOKA,JE YUPO TAYARI KUJIUNGA NA MAN U??''




















Winga wa Real Madrid Angel Di Maria,26 ameiambia klabu hiyo ya Hispania anataka kuondoka.Di Maria ambaye amehusishwa na uhamisho wa kwenda Manchester United,huku Van Gaal akionesha yuko makini kuhakikisha ananasa saini ya winga huyo.
KWA HABARI ZAIDI>>>