Sunday, 21 September 2014

"VAN GAAL ASHANGAZWA NA KICHAPO CHA GOLI 5 DHIDI YA LEICESTER 5-3 MAN U"






















Leicester city waliotokea nyuma wakiwa wamefungwa goli 3-1,wameibuka kidedea leo dhidi ya Manchester United.Man U walipata pigo baada ya mchezaji wao Blackett kupewa kadi nyekundu.Kwa upande wa Man u pazia la magoli lilifunguliwa na RVP dakika ya 13,Di Maria dakika ya 16,Herrera 57,Kwa upande wa wenyeji magoli yao yalifungwa na Ulloa (17 na dakika ya 83 (penati),Nugent dakika ya 62 (kwa penati).Cambiasso 64 na Vardy dak ya 79.

Saturday, 20 September 2014

"REAL MADRID YAUA 8,HUKU CR7 AKIPIGA HAT-TRICK",LIVERPOOL NAYO YACHEZESHWA KWATA NA WESTHAM,WHU 3-1 LFC"
















Cristiano Rolnado leo ameifungia timu yake magoli matatu huku vigogo hao wa soka wa hispania wakishinda goli 8 ugenini dhidi ya timu ya Deportivo La Coruna ambao walijipatia ushindi wa goli 2,CR ametia nyavuni dakika ya 29,48 na 78,James Rodriguez ameifungia timu yake dakika ya 36,Gareth Balle nae akifanikiwa kufumania nyavu mara 2,katika dakika ya 66 na 74,wakati huo Chicharito akifanikiwa kufumania nyavu mara mbili katika dakika ya 88.


Nao majogoo wa London wanaendelea kuchechemea kwa kukubali kichapo cha goli 3 dhidi ya West Ham United huku Liverpool wakifanikiwa kupata goli moja kupitia kwa mchezaji Sterling.Mambo yalionekana kuwaendea kombo dakika ya kwanza tu ya mchezo.Goli la Reid na Diafro Sakho yaliwapa nguvu West ham kumiliki sehemu kubwa ya  mchezo.




Friday, 19 September 2014

"KUTANA NA BABA WA WATOTO 26 'ANAEHUBIRI' KUHUSU UZAZI WA MPANGO"


























Katika nchi nyingi,ni  kawaida kwa mwanamke hasa maeneo ya vijijini kufanya kazi zaidi ya waume zao,ilhali wanaume wanapata muda mwingi wa kupumzika.Kutokana na uzoefu wa Kouayou almaarufu "Nabii".Anasema "Kwa utamaduni wetu,jinsi unavyopata watoto wengi,ndivyo unavyokua tajiri na mwenye ufahari nami nimeweka rekodi hiyo kijijini kwangu".


" WALIOKUFA KARNE 7 ZILIZOPITA WAKUTWA "WAMESHIKANA MIKONO ''






















Dunia ina mambo hata kifo kimeshindwa kuwatenganisha hawa wanaosadikiwa kufa miaka 700 iliyopita baada ya timu ya mambo ya kale kugundua uwepo wa kaburi hilo katika mji wa Leicester,walikuta wawili hao wakiwa wameshikana mikono.

Sunday, 14 September 2014

"MWENYE HIV AAMURIWA NA MAHAKAMA KUACHA KUWAAMBUKIZA WATU KWA MAKUSUDI"






















Jaji wa mahakama ya Seatle nchini Marekani ameamuru kijana anaetambulika kwa jina la "AO",aache mara moja kueneza ugonjwa na kwenda kupata tiba mara  moja,baada ya kuwaambukiza watu nane (8) ndani ya miaka minne (4).Ametakiwa kwenda kuwaona wataalamu wa maswala ya Ushauri ili kuwalinda wapenzi wake wengine dhidi ya  maambukizi.


Saturday, 13 September 2014

"ATLETICO MADRID WAENDELEZA UBABE KWA REAL MADRID, HUKU NEYMAR AKITUPIA 2''






















Watemi wa soka nchini Hispania wamekubali kichapo cha goli 2-1,dhidi ya wapinzani wao Atletico Madrid,wababe hao waliopata  goli kupitia kwa Cristiano Ronaldo aliefunga kwa penat Dakika ya 26,Magoli ya Atletico Madrid yamefungwa na Tiago katika dakika ya 10 huku la ushindi likifungwa na Turan katika dakika ya 76.

KWA HABARI ZAIDI>>>

NDANI YA NOU CAMP
Neymar aamsha mashabiki wake mara mbili,Neymar aliyetokea Benchi alifanikiwa kufunga magoli 
mawili,katika dakika ya 79 na 84,wakicheza na timu iliionesha ushindani mzito Athletic Bilbao





















KWA HABARI ZAIDI>>>



"COSTA ATUPIA HAT-TRICK,CHELSEA YAPAA HUKU LIVERPOOL IKIKALISHWA ANFIELD"






















Diego Costa amefanikiwa kupiga goli zake 3 ndani ya mechi moja yaani ''hat-trick'' ,magoli hayo yamefungwa katika dakika ya 45,56,na 67 huku Loic Remy akifunga pazia kwa kufunga bao la 4 dakika ya 81.Huu ni ushindi wa 4 mfululizo hiyo inaendelea kuwathibitishia   ushindi wa 100% tangu kuanza kwa ligi hiyo.Huku magoli ya Swansea yakifungwa na Terry dakika ya 11,na Shelvey 86.

KWA HABARI ZAIDI>>

NDANI YA ANFIELD MAMBO SI SHWARI

Liverpool nao wameteleza kwa kukubali kuchapwa goli moja,wakiwa ndani ya uwanja wao wa Anfield walipofungwa goli la mapema katika dakika ya 9 lililofungwa na Gabriel Agbonlahor,ambao ushindi huo umeipeleka Aston Villa kwenye nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.