Sunday, 31 August 2014

"REAL SOCIEDAD YAMCHARAZA REAL MADRID 4 KWA 2"


Real sociedad imewakimbiza mchachaka Real maadrid kwa kuichapa jumla ya goli 4 kwa 2,Ramos alieanza kufunga katika dakika ya 5,ikifuatiwa na goli la Bale dakika ya 11,Huku Martinez akisawazishia timu yake dakika ya 35,Zurutuza dakika ya 41 na 65 huku Vela akimalizia kufunga katika dakika ya 75
KWA HABARI ZAIDI>>>

"LIVERPOOL YAUA 3 DHIDI YA TOT"




















Brendan Rogers ameiongoza timu yake kushinda dhidi ya Tottenham,huku akifikisha mechi ya 100 tangu kuanza kuwa kocha wa Liverpool ndani ya White Hart Lane.Sterling aliyefungua pazia kwa kuifungia goli la kwanza dakika ya 8,huku Gerad akifunga kwa penat katika dakika ya 49,na Moreno alimalizia kwa kufunga goli la 3.
                          KWA HABARI ZAIDI>>>

Saturday, 30 August 2014

"MAN CITY WAKALISHWA ETIHAD,MAN U WASHIKWA SHATI"




















Stoke city wamefanikiwa kuwaduwaza Man city kwa kuwachapa goli moja liliwekwa kimiani na Mame Biram Diouf mnamo dakika 58 ya mchezo,Man city walifanikiwa kuduwazwa wakicheza uwanja wao wa nyumbani.Wakati huo Man u wakikaribishwa na Burnley wamelazimishwa sare ya bila kufungana.


Friday, 29 August 2014

"JIONEE TIMU YAKO IMEPANGWA KUNDI GANI,HUKU LIVERPOOL IKIPANGWA NA BINGWA MTETEZI,R MADRID"




GROUPS

GROUP A

AtléticoAtlético(ESP)
JuventusJuventus(ITA)
OlympiacosOlympiacos(GRE)
MalmöMalmö(SWE)

GROUP B

Real MadridReal Madrid(ESP)
BaselBasel(SUI)
LiverpoolLiverpool(ENG)
LudogoretsLudogorets(BUL)

GROUP C

BenficaBenfica(POR)
ZenitZenit(RUS)
LeverkusenLeverkusen(GER)
MonacoMonaco(FRA)

GROUP D

ArsenalArsenal(ENG)
DortmundDortmund(GER)
GalatasarayGalatasaray(TUR)
AnderlechtAnderlecht(BEL)

GROUP E

BayernBayern(GER)
Man. CityMan. City(ENG)
CSKA MoskvaCSKA Moskva(RUS)
RomaRoma(ITA)

GROUP F

BarcelonaBarcelona(ESP)
ParisParis(FRA)
AjaxAjax(NED)
APOELAPOEL(CYP)

GROUP G

ChelseaChelsea(ENG)
SchalkeSchalke(GER)
SportingSporting(POR)
MariborMaribor(SVN)

GROUP H

PortoPorto(POR)
Shakhtar DonetskShakhtar Donetsk(UKR)
AthleticAthletic(ESP)
BATEBATE(BLR)


Tuesday, 26 August 2014

"MABINTI WA UMRI WA MIAKA 5 WANAOZWA ILI KUJIKWAMUA NA UGUMU WA MAISHA"

Mmoja wa wanaume katika ndoa na binti aliye chini ya miaka 19,huu ni mfano tu wa ndoa hizo nchini Ethiopia.






















Nchini Ethiopia wazazi wanaoshindwa kuzihudumia familia zao huwaoza mabinti zao katika umri mdogo sana,hali hiyo huwapelekea vifo vya mimba za utotoni.Mwanamke mmoja anaejulikana kama Merkedes Murgeta ambaye hakumbuki hata tarehe ya ndoa yake,lakini ndugu zake wanamkumbusha kwamba aliolewa akiwa na miaka mitano (5).


Mugeta anaeishi katika kijiji cha Mosebo kilichopo mkoani Amhara katikati ya nchi ya Ethiopia.Katika eneo hili kama ilivyo kawaida kwenye maeneo mengine ya Ethiopia,ni kosa kuolewa chini ya miaka 18.Kutokana na takwimu za USAID,Amhara inatajwa kama sehemu ambapo ndoa za utotoni zimekithiri kuliko maeneo yote duniani.


"VIPAUMBELE VYA WANASIASA" 
"Nchi imeweka kipaumbele kikuu kwenye afya ya mama mjamzito na mtoto" 

Monday, 25 August 2014

"BIASHARA YA NYAMA YA PANYA INAWAINUA WENGI NCHINI CAMBODIA"

Panya wanaotegwa kutoka mashamba ya mpunga,inafikiriwa kuwa ni bidhaa adimu nchini Cambodia.

Mavuno ya kipekee yanayoendelea kwenye mashamba ya mpunga nchini Cambodia ambapo makumi elfu ya panya pori wanategwa wakiwa hai  kila siku,huku wakisafirishwa kwenda nje ya nchi hiyo.


LADHA YAKE NI SAWA NA KITIMOTO

Baadhi ya watumiaji wa nyama hiyo ya panya wanasema inafanana na ladha ya nyama ya Nguruwe,maarufu kama Kitimoto kama inavyotambulika katika baadhi ya maeneo mengi ya nchini Tanzania.








Sunday, 24 August 2014

"WAFUNGWA WAISHTAKI SERIKALI YA BOTSWANA KUDAI HAKI YA KUPATIWA ARV"


Mahakama kuu ya Nchini Botswana imeamuru serikali ya nchi hiyo kuwapatia dawa za kupunguza makali ya Virusi vya ukimwi,raia wote wa kigeni wanaotumikia vifungo kwa makosa mbalimbali nchini humo na gharama zote ziwe ni juu ya serikali ya  nchi hiyo.

    Hali hiyo imefuatia baada ya raia wawili wa Zimbabwe,Dickson Tapela na Mbuso Piye wanaotumikia kifungo nchini Botswana kuishtaki serikali hiyo kwa kukataa kuwapatia huduma ya dawa za kupunguza makali ya ukimwi.