Tuesday, 9 September 2014

"UNYANYASAJI MAJUMBANI,UNAUA ZAIDI YA VITA YA WENYEWE KWA WENYEWE''


























Ripoti ya Umoja wa Mataifa  imeweka bayana kwamba wengi wanakufa kutokana na ukatili wa nyumbani kuliko wanavyokufa kwenye uwanja wa mapambano,inayopelekea mamilioni kupotea kutokana na vifo hivyo vinavyosababishwa na ukatili majumbani.

  Ripoti hiyo inaendelea kuweka bayana kwamba Ukatili majumbani hasa unaowalenga Wanawake na Watoto,unauwa watu wengi kuliko athari halisi zinazotokana na Vita hiyo,inayogharimu dunia Dola Trilioni 8 kwa mwaka.....!!!

    
                                KWA HABARI ZAIDI>>>




Saturday, 6 September 2014

"WALIOFUNGWA KIMAKOSA KUTOKANA NA KESI YA UBAKAJI WAFIDIWA DOLA ZA KIMAREKANI MILION 41"


Jaji wa mahakama ya rufaa ya  ameamuru malipo ya Dola za kimarekani milioni arobaini na moja ($41) Kutoka Jiji la New York kulipwa kwa vijana watano waliotumikia kifungo cha miaka 30 jela  kimakosa baada ya kushtakiwa kwa kosa la ubakaji mwaka 1989.Malipo hayo ni fidia kwa wahanga au kuwafuta machozi, baada ya mwaka 2002 mtuhumiwa aliyetenda kosa hilo kukiri makosa hayo.


Friday, 5 September 2014

"SHIRIKA LA AFYA DUNIANI LASHAURI KUTUMIA DAMU ZA WALIOPONA EBOLA KUTIBU EBOLA"

Damu iliyotoka kwa watu waliopona Ebola yaweza kutumika ili kutibu wagonjwa wa Ebola...!!

Ule usemi wa dawa  ya moto ni moto unaotumiwa sana na waswahili nadhani unaweza ukakubaliana na hili tamko lilitolewa na Shirika la afya duniani ya WHO limetangaza kwamba "Damu za watu waliopona kutokana na maambukizi ya Ebola inapaswa itumike kuwatibu wagonjwa wapya walioathiriwa na ugonjwa huo".

Afrika Magharibi ndiyo imepata madhara makubwa tangu ugonjwa huo uanze kuenea katika ukanda huu zaidi ya watu 2000 wameshapoteza maisha.























"GOLI KIPA ALIYEINGIA KWENYE KITABU CHA GUINESS,HUYU SI MWINGINE NI ASMIR BEGOVIC"






















Huyo si mwingine bali mlinda mlango wa timu ya Stoke City Asmir Begovic,ambaye jina lake limefanikiwa kuandikwa katika kitabu cha rekodi za dunia cha Guiness baada ya kufunga goli la mbali sana.Alifunga goli hilo kwenye mechi iliyopigwa mwezi Novemba mwaka jana kati ya Stoke City na Southampton iliyoisha kwa suluhu ya 1-1,Alifunga goli hilo akiwa umbali wa mita 91.9 toka lango la wapinzani.

                                   KWA HABARI ZAIDI>>>

"KATIKA KARNE YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA,MAJI NI ANASA NA SIO HITAJI LA MUHIMU LA BINADAMU"

Baada ya miaka 30 ya njaa iliyokithiri nchini Ethiopia,bado upatikanaji wa maji ni wa mashaka hasa ukizingatia umuhimu weneyewe wa maji kwa binadamu kama usemi maarufu usemao maarufu ''MAJI NI UHAI''.Ikiwa asilimia 52 ya watu wote inapata huduma bora za maji lakini,asilimia 10 pekee ndio waliounganishiwa bomba hadi majumbani mwao.Katika maeneo ya vijijini ni asilimia 1 tu  iliyounganishwa na huduma hii muhimu katika maisha ya binadamu..


KWA HABARI ZAIDI>>>

Hii ina maana kubwa sana.Kwa nchi ambayo uchumi wake unategemea Kilimo,upungufu wa maji hauathiri Uchumi pekee bali  unaathiri maisha ya kila siku ya wakazi hawa ambao kujikimu kwao kunategemea mavuno ya kila msimu.Mara nyingi nchi maskini kama ya Ethiopia,yenye wakazi wengi,inakumbwa sana na janga la kukosekana kwa huduma ya maji.


Kuna mambo mengi yanayochangia ukosefu wa maji safi na salama,kuanzia uharibifu wa Mazingira unaosababishwa na ukataji ovyo wa miti,majanga ya kiasili kama Mafuriko na mabadiliko ya tabia nchi....!!!


Thursday, 4 September 2014

"ABIRIA KADHAA WAHOFIWA KUFA BAADA YA BASI KUSOMBWA NA MAFURIKO"


Takribani abiria 70 wanahofiwa kufa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kusombwa na mafuriko katika jimbo la Kashmir,inaripotiwa.Ajali hiyo iliyotokea Alhamisi Kusini mwa Wilaya ya Rajouri katika ukanda wa Himalaya ambapo imekumbwa na mafuriko makali tangu miaka 22.

Wednesday, 3 September 2014

"HII INAUMA,JAMAA WAKUTWA HAWANA HATIA BAADA YA KUFUNGWA JELA KWA MIAKA 30"


Vipimo vya vinasaba vilionesha ndugu hao wawili,ambao wana matatizo ya akili pia walikua ni vijana wadogo chini ya umri wa miaka 20,walioingia hatiani kimakosa tangu 1983.Wawili hao waliachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha miaka 30 ikiwa ni sawa na Miongo mitatu,jela kwa kesi ya Ubakaji na Mauaji ya binti wa miaka 11 baada ya ushahidi kuwekwa wazi kupitia vipimo vya vinasaba.Machungu na manung'uniko yao hayatakwisha kamwe.