Sunday 12 October 2014

"KIMBUNGA HUD HUD CHALETA MAAFA NCHINI INDIA''

  Kimbunga cha Hud Hud kinaendelea kimeuvuruga ukanda wa mashariki wa India,na kusababisha uharibifu uliopelekea kuwaondoa watu 350,000 kama hatua za usalama kwa raia hao.

   Hata hivyo inasemekana watu watatu wamekufa katika mji Andhra Pradesh na watatu pia katika mji wa Orissa.Kimbunga hicho kilichowekwa kwenye kundi ''Madhara sana'' kimeleta upepo uliokuwa unasafiri kwa mwendo kasi wa kilometa 205 kwa saa (205Km/h),kilivyokua kinapita pwani ya karibu na jiji la Visakhapatnam.Upepo huo mkali na mvua zimesababisha uharibifu wa miti,kukatika kwa huduma ya umeme pia uharibifu wa mazao shambani na majengo katika miji yote miwili.


KWA HABARI ZAIDI>>>

No comments:

Post a Comment