Tuesday 14 October 2014

"KAMA KUBUSU TU UNAFUKUZWA KAZI,JE UKILA RUSHWAAA ITAKUAJE''

ASKARI WAKIWA WANAPEANA MABUSU MOTO MOTO MUDA WA KAZI.

Ni muda upi ambao ni muafaka kwa wewe kumbusu rafiki au mtu wako wa karibu?,Picha hapo juu inaonesha askari wawili wakipigana busu lililopelekea wao kupoteza kazi ''KWA AJILI YA BUSU TU?''.Kwa mtazamo wa kawaida hawa askari wawili hawakufikiria kama swala lingefika hatua mbaya ya kupelekea kufukuzwa kazi.Picha hiyo iliyopigwa Kagera-Kaskazini Magharibi mwa Tanzania-Ikionesha wawili hao wakipeana busu huku wakiwa wamevalia unifomu za kazini na hicho tu kilichukuliwa kama kigezo cha kuwafukuza kazi.

Picha hiyo iliyopakiwa kwenye intanenti na askari wa tatu,ambaye ndiye aliyepiga picha hiyo,iliyoibua mamlaka husika kulivalia njuga swala hilo,ndani ya Mamlaka ya Polisi mjini Kagera.Henry Mwaibambe ambaye ni Kamanda wa Polisi Mkoa akiongea na BBC kuhusu hatua zilizochukuliwa,na kutetea maamuzi ya idara.Ingawa kwenye mitandao mingi ya kijamii watu wengi wamekua na maoni tofauti" niliwahi kuona picha ya aliyekua Raisi wa Marekani Reagan akimbusu mke wake,na hakuna aliyetaka kumwajibisha'',Mwingine akaongezea kwa kusema "Akari wawili wanapobusiana adhabu yao ni kubwa kuliko wala rushwa"
















No comments:

Post a Comment