Sunday, 14 December 2014
Saturday, 15 November 2014
"MTOTO WA MIAKA 5 AFAULU MTIHANI WA MICROSOFT"
Mtoto huyo anaetokea Coventry amekua ndiye mtu mwenye umri mdogo sana kuwa na ujuzi wa maswala ya Computer duniani.Mtoto huyo anaekwenda kwa jina la Ayan Qureshi sasa ni Microsoft Certified Proffessional (MCP) baada ya kufaulu mtihani wa kiufundi unaotungwa na na kuratibiwa na Microsoft akiwa na umri wa miaka mitano (5) tu.
Ayan ambae kwa sasa ana miaka 6,baba yake ni mtaalamu na mshauri kwenye maswala ya teknolojia,ametengeneza mtandao wa komputa nyumbani.
Wednesday, 29 October 2014
"KUTANA NA KIJANA ANAYETENGENEZA MAMILIONI YA PESA KWA KUSAFISHA VIATU"
Haijalishi ni aina gani ya viatu gani unavaa katika mkutano muhimu wa biashara swala kubwa la msingi ni viwe vinang'aa na vyenye mvuto.Picha juu hapo inaonesha kijana aliyekuwa maarufu kwa uuzaji wa Mayai akifanya kazi yake ya 'Shoe Shiner'.Kijana huyo anaekwenda kwa jina la Lere Mgayiya anasema wana kampuni kubwa ya kusafisha viatu kwa Afrika nzima,"Wakiwa ndani ya Johansburg wanasafisha pea 350 kwa siku ,Pea 120 Capetown,na 120 zingine kutoka Durban.Kampuni yake imeajiri wafanyakazi 45 ambao kwa sasa wametawanyika kwenye Viwanja vya ndege vitatu.Hadi sasa ana utajiri wa Randi Milioni 2.5 sawa na Dola 227,000 kwa kazi hiyo....
Thursday, 16 October 2014
"USHAWAHI KUONA MASHINDANO YA NDEVU?",ANGALIA WATU NA NDEVU ZAO NI SHEEEEDA...!!
Dunia ina mambo na vijambo,ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni,duniani watu tumezoea kuona mashabiki wa fani mbalimbali ikiwemo Mpira wa Miguu,gofu,nk.Ila mwaka huu 25/10/2014 kutakuwa na shindano maarufu la "NDEVU NA MUSTACHI",litakalofanyika Portland,Oregon.Inatarajiwa watu 3000 ''Wenye Ndevu'' kuhudhuria shindano hilo na watashindana katika vipengele mbalimbali....!!!
Tuesday, 14 October 2014
"KAMA KUBUSU TU UNAFUKUZWA KAZI,JE UKILA RUSHWAAA ITAKUAJE''
Sunday, 12 October 2014
"KIMBUNGA HUD HUD CHALETA MAAFA NCHINI INDIA''
Kimbunga cha Hud Hud kinaendelea kimeuvuruga ukanda wa mashariki wa India,na kusababisha uharibifu uliopelekea kuwaondoa watu 350,000 kama hatua za usalama kwa raia hao.
Hata hivyo inasemekana watu watatu wamekufa katika mji Andhra Pradesh na watatu pia katika mji wa Orissa.Kimbunga hicho kilichowekwa kwenye kundi ''Madhara sana'' kimeleta upepo uliokuwa unasafiri kwa mwendo kasi wa kilometa 205 kwa saa (205Km/h),kilivyokua kinapita pwani ya karibu na jiji la Visakhapatnam.Upepo huo mkali na mvua zimesababisha uharibifu wa miti,kukatika kwa huduma ya umeme pia uharibifu wa mazao shambani na majengo katika miji yote miwili.
KWA HABARI ZAIDI>>>
Saturday, 4 October 2014
"MCHUNGAJI WA AINA HII KAA NAE CHONJO"
Hiki ni kipande cha tukio la mchungaji aliyefumaniwa hotelini na mwanadada mrembo imeleta mkanganyiko pia imepelekea sintofahamu kwa wakazi nchini Kenya.Ilirushwa katika kipindi cha taarifa ya habari ya Kenya,ilionesha mchungaji wa kanisa la Anglikana Charles Githinji akiwa amevalisha sehemu tu ya mwili wake,akiwa na msichana binti mrembo.Huku anaedaiwa kuwa na mume wa msichana mrembo akiingia na timu ya watu wa televisioni na kamera kushuhudia tukio hilo..
Subscribe to:
Posts (Atom)